Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pillay ataka pande Zinazozozana nchini Syria Kuzuia Mauaji ya raia

Pillay ataka pande Zinazozozana nchini Syria Kuzuia Mauaji ya raia

Huku mapigano yakiwa yanaendelea katika karibu kila sehemu nchini Syria, mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay amezitaka pande husika kuwa makini na kuhakikisha kuwa hakuna vifo vya raia kwenye mapigano hayo.

Pillay anasema kuwa ghasia zinazoendelea hasa mijini ni hatari kwa usalama wa raia akiongeza kuwa watu wasiokuwa na hatia tayari wameuawa na kujeruhiwa na wengine mamilioni kulazimika kuhama makwao. Rupert Colville ni msemaji wa ofisi ya Haki za Binadamu 

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)