Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UNHCR asikitishwa na Idadi ya Watu Walokimbia ghasia Syria

Mkuu wa UNHCR asikitishwa na Idadi ya Watu Walokimbia ghasia Syria

Kamishna mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, leo ameelezea hofu yake kuhusu idadi ya watu wengi kupindukia wanaokimbia makwao kwa ajili ya ghasia zaidi nchini Syria.

Maelfu ya raia wa Syria walivuka mpaka na kuingia Lebanon hapo jana. Duru za habari zinasema kati ya watu 8, 500 na 30, 000 wamevuka mpaka huo katika saa 48 zilizopita. Inakadiriwa pia kuwa idadi kubwa ya watu wamelazimika kuhama makwao kama wakimbizi wa ndani, wengi wao wakiishi mjini Damascus. Shirika la UNHCR, kwa kushauriana na serikali na wadau wengine, linajaribu kuhakiki idadi kamili ya watu ambao wamelazimika kuhama makwao au kuvuka mipaka.

Kwa sasa huduma za UNHCR zinaangazia kuwasaidia wakimbizi ambao wana mahitaji ya dharura zaidi, kama wale wasio na makazi mjini Damascus. Melissa Fleming ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA MELISSA FLEMING)