Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Libya sasa inapaswa kusonga mbele Kukumbatia Mabadiliko ya Kidemokrasia:UM

Libya sasa inapaswa kusonga mbele Kukumbatia Mabadiliko ya Kidemokrasia:UM

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, amesifu mafanikio yaliyofikiwa kwenye uchaguzi uliopita na amehimiza taifa hilo kuanza kuchukua mkondo wa kusonga mbele na kuhakikisha ukabidhiji madaraka kwa njia ya kidemokrasia unaendelea unasalia kioo cha siku za usoni.

Akitoa taarifa yake mbele ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa Ian Martin amesema kuwa taifa hilo sasa linapaswa kukubaliana namna ya kuunda serikali mpya itayotimiza matakwa ya wote.

Wananchi wa Libya waliteremka kwenye vituo vya kupigia kura tarehe 7 July katika uchaguzi ambao umepongezwa na jumuiya za kimataifa.