Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa Walaani Matukio ya Ubakaji DRC

Umoja wa Mataifa Walaani Matukio ya Ubakaji DRC

Afisa wa Umoja wa Mataifa amelaani vikali vitendo vya unyanyasaji wa kingono unaodaiwa kufanywa na vikosi vya wanamgambo huko mashariki wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo DRC ambao pia wameendesha hujuma nyingine kwa maguruneti.

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kwenye maeneo yaliyokumbwa na mizizo Vijay Nambiar amehimizwa kuanzishwa uchunguzi wa haraka dhidi ya vikosi hivyo vya M23 ambavyo vinaendesha shabaha ya kuteka maeneo muhimu.

Duru za habari zinaarifu kuongezeka kwa mashambulizi kunakokwenda sambamba na matukio ya manyanyaso ya kingono na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Katika maeneo kadhaa ikiwemo kijiji cha Epulu vikosi vya waasi kwenye eneo hilo vijulikanavyo kama Mai Mai Simba, vimeripotiwa kufanya ubakaji kwa wanawake kadhaa na kuwateka wengine kadhaa kwa ajira ya kuwatumikisha katika vitendo vya kingono.