Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Marekani Yaunga Mkono juhudi za Kukabiliana na Tatizo la Njaa Duniani

Marekani Yaunga Mkono juhudi za Kukabiliana na Tatizo la Njaa Duniani

Ikizitizama changamoto ambazo zinaendelea kuchukua sura ya kuongezeka, Marekani imeweka shabaha yake kuongeza umakini wa kukabiliana na majanga ya kimaumbile yanayoendelea kuikabili dunia kwa wakati huu.

Marekani umekubali kuongeza mashirikiano na mgango wa chakula duniani WFP na imehaidi kutoa kiasi cha dola milioni 864.5 ikiwa ni fedha taslimu na chakula ili kuwasaidia watu wanaokabiliwa na mkwamo wa chakula.

Takwimu za FAO zinaonyesha kuwa mamilioni ya watu walioko katika mataifa 37 wapo kwenye mkwamo mkubwa wa chakula kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo maeneo mengine kukabiliwa na tatizo la ukame.

Katika makabidhiano hayo, serikali ya Marekani imesema kuwa inachukua hatua muhimu kuunga mkono juhudi zozote zinazochukuluwa ili kuwafikia watu hao walioko kwenye mahitajio ya chakula.