Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yaongeza juhudi za Kukabiliana na Wadudu wabaya wa Nyanya Mashariki ya Kati

FAO yaongeza juhudi za Kukabiliana na Wadudu wabaya wa Nyanya Mashariki ya Kati

Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa, FAO, linaongeza juhudi zake za kupambana na wadudu wanaoathiri mmea wa nyanya eneo la Mashariki ya Kati. Pamoja na wadau wengine, shirika la FAO linasisitizia matumizi ya mipango isiyoathiri mazingira ya kuzuia wadudu hao wanaoguguna nyanya, ambayo tayari imepata ufanisi kupunguza uharibifu wa wadudu hao kwenye bahari ya Mediterranea na baadhi ya mataifa ya Afrika Kaskazini.

Mipango inaendelea kwa sasa, kwa ajili ya mradi wa kikanda wa kuwadhibiti wadudu hao waitwao Tuta absoluta katika mataifa ya Misri, Iran, Iraq, Jordan, Lebanon, Syria na Yemen, kufuata mbinu iliyotumiwa katika eneo la Mediterranea. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)