Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maendeleo ya Uchina na Afrika yatatokana na Ushirikiano katika Uchumi wa Kimataifa:Ban

Maendeleo ya Uchina na Afrika yatatokana na Ushirikiano katika Uchumi wa Kimataifa:Ban

Mtazamo wa sasa ni kuwa maendeleo ya Uchina na mataifa ya bara la Afrika yatatokana na kushirikiana katika uchumi na soko la kimataifa, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon.

Bwana Ban amesema hayo leo, wakati akilihutubia kongamano la tano la mawaziri kuhusu ushirikiano wa Uchina na bara la Afrika mjini Beijing. Akitaja kuwa ushirikiano kati ya Uchina na bara Afrika umetoka siku za jadi, amesema ushirikiano wa sasa ni wa malengo muhimu, kwa ajili ya siku zijazo.

Ameongeza kuwa ushirikiano wa sasa wa usawa na manufaa kwa wote, umepea, na kwamba sasa Uchina imekuwa mshirika muhimu wa biashara na bara la Afrika.