Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNMISS ipo Kuwasaidia Watu wa Sudan Kusini:Hilde Johnson

UNMISS ipo Kuwasaidia Watu wa Sudan Kusini:Hilde Johnson

Mwakilishi maalum na mkuu wa uangalizi wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini, yaani UNMISS, Hilde Johnson, amesema vikosi vya Umoja wa Mataifa vitaingilia kati na kuchukuwa hatua iwapo maisha ya raia yatawekwa hatarini.

Bi Johnson amesema hayo wakati wa ziara yake kwenye jimbo la Equatoria la Sudan Kusini, ambako amesema kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Mataifa kutoka Rwanda kimeanza kushika doria katika baadhi ya maeneo ambayo awali yaliathiriwa na waasi wa LRA.

Amesema ziara ya ujumbe wa UNMISS kwenye jimbo hilo pia imewapa ari ya kushirikiana na vikosi mbalimbali vilivyopo katika eneo hilo,  vya Muungano wa Afrika, jeshi la taifa la Uganda au washauri wa kijeshi wa Marekani.