Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Angola yafanya Mikakati ya Kuhitimu kutoka kwa Mataifa Maskini zaidi duniani

Angola yafanya Mikakati ya Kuhitimu kutoka kwa Mataifa Maskini zaidi duniani

Serikali ya Angola inaelekea kukamilisha ripoti inayooesha hatau ambazo itachukua ili kujiondoa kwenye orodha ya mataifa yanayoorodheshwa kuwa maskini zaidi duniani. Shirika la biashara na mandeleo la Umoja wa Mataifa UNCTAD pamoja na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa yataisaidia Angola katika kukagua hatua zitakazoiwezesha kuhitimu.

Ikiwa Angola itakuwa imetimiza viwango vinavyohitajika kabla ya kukaguliwa tena kwa mataifa maskini zaidi duniani mwaka 2015 kamati ya CDP itapendekeza kuhitimu kwake kutoka orodha ya mataifa maskini . Jason Nyakundi na maelezo zaidi.

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)