Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wataka Kusimamishwa hatua ya Kunyongwa kwa Watuhumiwa wawili wa Mauaji nchini Marekani

UM wataka Kusimamishwa hatua ya Kunyongwa kwa Watuhumiwa wawili wa Mauaji nchini Marekani

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu masauala ya kunyongwa kuzikozingatia sheria Christof Heyns ameutaka usimamizi wa majimbo ya Georgia na Texas nchini Marekani kuzuia kunyongwa kwa watu wawili wanaokisiwa na kuwa matatizo ya kisaikolojia wanapangiwa kunyongwa hii leo.

Warren Hill na Yomamon Laneal Hearn walipatikana na hatia ya kuua kwenye visa tofauti. Heynes amasema kuwa hatau hiyo ni ukiukaji wa sheria inayohusu hukumu ya kifo kwa kutoa hukumu kama hiyo kwa watu walio na matatizo ya kisaikolojia. Mtaalamu huyo maalum ametaka tawala za majimbo hayo kuonyesha kile alichokitaja kuwa umuhimu wa haki ya kuishi. Ameonya kuwa huenda serikali zingine zinakafauata mfano kama huo wa kuwahukumu watu wanaokabiliwa na matatizo ya kisaikolojia.