Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya Wakimbizi wa Syria Imeongezeka Maradufu:UNHCR

Idadi ya Wakimbizi wa Syria Imeongezeka Maradufu:UNHCR

Kuna ripoti kwamba idadi ya wakimbizi wa Syria walioandikishwa katika nchi za Iraq, Jordan, Lebanon na Uturuki imeongezeka mara dufu na sasa inakadiriwa kufukia 112,000.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema kuwa kiasi kikubwa cha wakimbizi hao ni wanawake na watoto na kwamba idadi hiyo inaweza kupindukia katika siku za usoni.

Katika mataifa yote manne ambayo yamepokea wakimbizi hao, UNHCR inasema kuwa makundi hayo ya watu yanasalia kutegemea misaada ya dharura.

Nchini Jordan UNHCR imesema wakimbizi waliandikishwa wanafikia 33,421 ikiwa imezidi wale walioandikishwa huko Iraq ambao ni 29,091.