Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yataka Mafungu ya Fedha kuratibu Makundi ya wahamiaji

IOM yataka Mafungu ya Fedha kuratibu Makundi ya wahamiaji

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji limetaka kupatiwa mafungu ya fedha ili kuwahudumia mamia ya wahamiaji ambao sasa wanaanza kurejea kwa wingi nchini Libya baada ya kuwa uhamishoni wakikimbia machafuko yaliyolikumba taifa hilo.

IOM imesema kuwa kuna idadi kubwa ya wahamiaji kutoka Chad wanaoingia kwa wingi nchini Libya kwa shabaha ya kusaka kazi na maisha bora.

Shirika hilo limeitaka jumuiya ya kimataifa kutoa mafunga ya fedha ili kufanikisha mpango wa kuwafungamanisha wahamiaji hao katika jamii ya kawaida hasa lakini katika maneo yale ya mipakani ambako kuna kundi kubwa la watu wanaowasili.

Hivi karibuni serikali ya Chad iliomba IOM kusaidia kuwakwamua makundi kadhaa ya watu kurejea makwao baada ya jaribio lao la kuvuka mpaka na kuingia Libya kushindikana.