Mfanyakazi wa WHO Ajeruhiwa nchini Pakistan

17 Julai 2012

Mfanyakazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) na mtaalam mmoja wa kimataifa wamejeruhiwa wakati gari lao liliposhambuliwa na watu wenye silaha mjini Karachi, Pakistan. Katika taarifa yake, WHO imesema hali za watu hao wawili ambao walikuwa wakifanya kwenye huduma ya WHO si mbaya sana.

Wawili hao walikuwa wakisaidia mkakati unaoendelea nchini humo wa kuwapa watoto chanjo dhidi ya ugonjwa wa kupooza. Hakuna ushahidi wowote kwa sasa unaoonyesha kuwa mashambulizi haya yalikusudiwa kulenga WHO, au kupinga juhudi zake za kutokomeza ugonjwa wa kupooza. WHO imeishukuru serikali ya Pakistan kwa kuanzisha uchunguzi katika tukio hili, na kutambua ni nini hasa kiini cha mashambulizi hayo.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter