Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waangalizi wa UM watembelea eneo la Mauaji nchini Syria

Waangalizi wa UM watembelea eneo la Mauaji nchini Syria

Waangalizi wa Umoja wa Mataifa ambao wamefanya ukaguzi katika kijiji cha Tremseh nchini Syria siku ya jumapili, wamesema kulingana na kile walichokiona na ushahidi uliopo, mashambulizi ya Julai 12 yalilenga waasi wa kijeshi na wanaharakati.

Wafanyakazi kutoka mpango wa Umoja wa Mataifa, UNSMIS, walishuhudia zaidi ya nyumba 50 kuchomwa au kuharibiwa na wamebaini kuwa damu nyingi na bongo zilipatikana katika maeneo ya makazi mengi.

UNSMIS imesema ushahidi uliotolewa na wanakijiji 27 waliohojiwa na timu ya Umoja wa Mataifa, umeonyesha kuwa mashambulizi yalianza vijijini mapema kutoka kwa mabomu na kufuatiwa na shughuli za ardhini.

Hii ni kulingana na Kiongozi wa timu ya maoni wa Norway hapo Jumapili.

Tuliingia kijiji cha Treimseh kuangalia baadhi ya maeneo ya majengo yaliyoharibiwa na mabaki ya vita na mashambulizi yaliyofanyika juzi. Hadi sasa tumeona idadi ya kubwa ya majengo yaliyochomwa na pia tumeona mabaki ya vita kama vile pesa , mashimo ya risasi ….