Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashambulizi katika kijiji Syria yalilenga Vikosi vya Waasi na Kazi zao:UM

Mashambulizi katika kijiji Syria yalilenga Vikosi vya Waasi na Kazi zao:UM

Ripoti iliyotolewa na waangalizi hao wapatao 50 inaonyesha kuwa vikosi vya serikali viliendesha msako wa nyumba kwa nyumba wakiulizia vitambulisho na baadaye waliwauwa wanavijiji hao na wengine waliwachukua sehemu isiyojulikana. Waangalizi hao wamesema pia kuna idadi kubwa ya majeruhi ambao bado hawajatambulika na jitihada zinachukiliwa ili kuwatambua.

Wakati hali ikiwa hivyo, mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan leo amewasili nchini Urusi kwa ziara ya siku mbili akijadiliana na viongozi wa taifa hilo juu ya mzozo wa Syria.