Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Antonio Guterres Akamilisha Ziara yake nchini Myanmar

Antonio Guterres Akamilisha Ziara yake nchini Myanmar

Mkuu wa shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR Antonio Guterres amekamilisha ziara yake ya siku mbili nchini Mynmar ambapo amewahakikishia kujitolea kwa Umoja wa Mataifa katika kutoa misaada ya kibindamu kwa watu kwenye jimbo la Rakhine bila ya ubaguzi.

Amesema kuwa hatua hiyo itachangia katika kuleta uiano kati ya jamii akiongeza kuwa kuna matumaini kuwa sheria itaanza kutekelezwa kwenye jimbo la Rakhine kwa kuzingatia haki za binadamu. Alielezea matumaini yake kwa rais na serikali ya Mynmar kuwa watu wa jamii ya waislamu watapewa utaifa kuambatana na sheria na kwa wengine wanaostahili kupata haki ya kuishi maisha ya kawaida.