Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pillay akaribisha Tangazo la Malaysia Kubadili Sheria ya Uchochezi

Pillay akaribisha Tangazo la Malaysia Kubadili Sheria ya Uchochezi

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu, Navi Pillay, amekaribisha tangazo la serikali ya Malaysia la kuiondoa sheria ya uchochezi katika katiba yake, na badala yake kuweka sheria ya itifaki au utungamano wa kitaifa.

Bi Pillay amesema sheria hiyo ya mwaka 1948, na ambayo ilikuwa ya kikoloni, ilibana uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa watu kujieleza nchini humo. Amesema kuwa kumekuwa na hofu awali kuhusu jinsi mabadiliko fulani ya kisheria hufanywa haraka bila kuwahusisha wananchi. Ametoa wito pia kwa serikali kuzihusisha taasisi husika za kitaifa, zikiwemo tume ya haki za binadamu ya Malaysia na raia wa nchi hiyo, na kuhakikisha kuwa sheria mpya ya utangamano itakwenda sambamba na viwango vya kimataifa vya haki za binadamu

Amesema ofisi yake i tayari kushirikiana na serikali hiyo katika mkakati mzima wa kufanya mabadiliko ya kikatiba.