Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Annan Alaani Vikali Mauaji ya Halaiki katika kijiji cha Tremseh Syria

Annan Alaani Vikali Mauaji ya Halaiki katika kijiji cha Tremseh Syria

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa na Umoja wan chi za Kiarabu kuhusu Syria, Kofi Annan, amelaani vikali mauaji ya zaidi ya watu 200 katika kijiji cha Tremseh, kati mwa jimbo la Hama nchini Syria. Katika taarifa yake mapema Ijumaa, Bwana Annan ameelezea mshtuko na masikitiko yake kufuatia habari za mapigano makali na idadi kubwa ya maangamizo, pamoja na matumizi ya silaha nzito nzito kama mizinga, makombora na mahelikopta.

Ametoa wito kwa serikali zenye ushawishi mkubwa kuweka shinikizo zaidi ili kuhakikisha ghasia zinakwisha mara moja. Amesema kwa kutumia silaha hizo nzito kwenye maeneo ya halaiki, serikali ya Syria inakiuka ahadi yake ya kitimiza mpango wa amani wa vipengee sita.

Mkuu wa waangalizi wa Umoja wa Mataifa Syria, UNSMIS, Meja Jenerali Robert Mood, amesema UNSMIS iko tayari kwenda kuhakiki hali halisi pale itakapoamini kuwa mapigano yamesitishwa, na kwamba wana uhakika kuwa bado kuwa mapigano katika eneo ya Treimsa.