Uchafuzi wa Hali ya Hewa kutokana na Matumizi ya Mafuta ya Petroli na Diesel

13 Julai 2012

Wakati ulimwengu unapojitahidi kwa kila njia kupunguza uchafuzi wa hali ya hewa na mabadiliko ya hali ya hewa bado kuna changamoto nyingi hasa kutokana na uchafuzi wa hewa unaotokana na gesi na vyombo vinavyototumia mafuta ya petroli na diesel. Hata kama nchi nyingi zimepiga hatua katika kuhakikisha kuwa yameondoa madini yanoyoathiri afya za wanadamu na mimea yakiwemo madini ya risasi yanayopatikana kwenye mafuta ya petroli, bado nchi zingine hazijafanikiwa katika kusafisha mafuta yao kwa viwango vya kumaliza madini hayo kabisa.

Kwa mfano nchi nyingi za bara la Afrika bado zimesalia nyuma katika kusafisha mafuta ikiwemo diesel ambayo pia ina kemikali ya Sulphur ambayo kwa njia moja au nyingine huathiri afya ya binadamu. Mwandishi wetu wa Nairobi Jason Nyakundi alipata fursa ya kuzungumza na mkuu wa kitengo cha usafiri kwenye shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa mjini Nairobi nchini Kenya UNEP Jane Akumu ambaye ameelezea kwa kina athari za madini kwenye mafuta na jitihada ambazo zimefanywa kukabiliana na tatizo hilo.

(MAHOJIANO YA JANE AKUMU NA JASON NYAKUNDI)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter