Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuzo ya Wangari Maathai yazinduliwa:FAO

Tuzo ya Wangari Maathai yazinduliwa:FAO

Shirika la Ushiirikiano Kuhusu Misitu (CPF), umetangaza tuzo ya Wangari Maathai, ambayo ni ya kwanza ya aina yake, kwa heshima na kumbukumbu ya mwanamke huyo mwenye uwezo wa ajabu, ambaye alikuwa mwanaharakati wa mambo ya misitu kote ulimwenguni.

Tuzo hiyo ya jumla ya dola 20, 000, itatolewa kwa mtu ambaye amefanya mchango mkubwa katika kuhifadhi, kuibua tena na kudhibiti misitu kwa njia endelevu, na kutoa mafunzo kuhusu umuhimu wa misitu katika maisha ya watu vijijini na mazingira katika vizazi vyote.

Washindani watakaguliwa jopo la watu maarufu kimataifa, ambao wataangazia masuala ya kuimarisha umma, kuchagiza kujitolea kwa kijamii, kuendeleza mitandao na kueneza ujumbe wa kuthamini misitu katika jamii. Tuzo ya Wangari Maathai itatolewa Septemba 27, ambayo ni tarehe ya kuadhimisha kifo chake mama huyo, wakati wa mkutano wa kamati ya Shirika la Chakula na Kilimo Duniani, FAO kuhusu misitu.