Annan ataka Kutekelezwa Mpango wa Amani wa Pande Sita nchini Syria

12 Julai 2012

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa na muungano wa nchi za kiarabu Kofi Annan hapo jana amesisitiza umuhimu wa kutekelezwa kwa mpango wa pande sita wa amani ili kusitisha ghasia zinazoendelea nchini Syria na kusema kuwa jamii ya kimataifa ni lazima ishirikina kuhakikisha ghasia nchini Syria zimekomeshwa.

Mapema leo Annan aliliarifu Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitia kwa njia ya video kuhusu ziara yake mjini Damascus mji mkuu wa Syria, ambapo alikutana na rais Bashar Al- Assad na kuhusu mikutano yake na viongozi wa Iran na Iraq alipofanya ziara maeneo hayo mapema juma hili.

Akiwahutubia waandishi wa habari mjini Geneva Annan amesema kuwa wakati wa mkutano wake na rais Al- Assad walikubaliana kuchukuliwa hatua za haraka kweneye maeneo yanayokumbwa na shasia mbaya wanapoendelea kujitahidi kutekeleza mpango wa pande sita wa amani uliowasilishwa na Annan mapema mwaka huu.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter