Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanafunzi wa UNRWA Wasaidiwa na Korea Kusini Kufungua Mawasiliano na Ulimwengu

Wanafunzi wa UNRWA Wasaidiwa na Korea Kusini Kufungua Mawasiliano na Ulimwengu

Serikali ya Korea Kusini, kupitia shirika lake la ushirikiano wa kimataifa (KOICA), imetoa tarakilishi 600 kwa wanafunzi wakimbizi wa Kipalestina kwenye Ukingo wa Gaza kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya wakimbizi wa Palestina, UNRWA. Tarakilishi hizo zitawasaidia takriban wanafunzi 30, 000 kupata mafunzo ya kompyuta na elimu ya mtandao.

Katika hotuba yake kwenye hafla ilofanyika katika shule ya UNRWA mjini Gaza, Mwakilishi Mkuu wa Korea Kusini Palestina, Sung Jun Yeo, amesema anaamini mradi huo utachangia kuendeleza mfumo wa elimu kwa wanafunzi hao, na kwamba msaada huo wa vyombo vya taaluma ya mawasiliano utawezesha vijana wengi zaidi wanaofuzu kuwa na ufahamu wa mambo kote ulimwenguni.