Afya ya Uzazi latajwa kuwa Tatizo kwa Wanawake Waliohitimu Umri wa Kuzaa

11 Julai 2012

Afya ya uzazi limetajwa kuwa tatizo linaloongoza kwenye vifo vya wanawake waliohitimu umri wa kuzaa duniani huku wanawake 800 wakiaga dunia kila siku wakati wanapojifungua. Pia karibu vijana bilioni 1.8 huwa wanahitimu umri wa kuzaa bila ya wao kufahamu huduma wazohitaji ili kujilinda.

Eneo lililo chini ya tume ya Umoja wa Mataifa kuhusu uchumi barani Ulaya linakabiliwa na changamoto nyingi zinazohusiana na masusla ya afya ya uzazi kwa mfano muungano wa nchi zilizokuwa chini ya utawala wa kisovieti kunaripotiwa vifo 23 kwa kila watoto 100,000 wanaozaliwa wakati kunaporitiwa vifo sita kwenye nchi zilizo kwenye muungano wa Ulaya. Jumla ya mataifa 179 yalitia sahihi mpango wa shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo na idadi ya watu na kutumika kwenye malengo ya maendeleo ya milenia mwaka 2000.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter