Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wenyeji wa Kaskazini mwa Mali Wanaelekea Kugumu Siku za Usoni:UM

Wenyeji wa Kaskazini mwa Mali Wanaelekea Kugumu Siku za Usoni:UM

Wajumbe wawili maalum wa Umoja wa Mataifa wameshutumu vikali ukikaji wa haki za kitamaduni na haki ya kuabudu kaskazini mwa Mali kufuatia kuharibia kwa sehemu za kuabudu likiwemo eneo la kitamaduni la Timbuktu. Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kuhusu masusla ya haki za kitamaduni Farida Shaheed anasema kuwa vitendo hivyo vinaashiria hali ngumu kwa wenyeji wa kaskazini mwa Mali siku za usoni.

Amesema kuwa uharibifu wa makaburi kwenye eneo la Timbuktu ambalo ni eneo maarufu la kitamaduni ni hasara kwa kila mmoja na kuwakosesha kitambulishao wenyeji, na hadhi yao. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)