Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waitaka Somalia kuanzisha mustakhabal mpya wakati muda wa serikali ya mpito ukikaribia kuisha

UM waitaka Somalia kuanzisha mustakhabal mpya wakati muda wa serikali ya mpito ukikaribia kuisha

Wakati kukaribia muda uliowekwa wa kufikia ukomo wa serikali ya mpito nchini Somalia, Umoja wa Mataifa umeelezea kile kinachopaswa kupiganiwa sasa na wananchi wa taifa hilo ambalo bado linashuhudia hali ya uhasama.

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini humo Augustine Mahiga amesema zingatio linalopaswa kutupiwa macho ni kuangalia hamta ya taifa hilo baada ya kukamilika kwa kipindi cha mpito. Serikali hiyo ya mpito inatazamiwa kufikia muhula wake wa mwisho ifikapo August mwaka huu lakini hata hivyo hali ya shaka shaka bado inaliandama taifa hilo.

Mjumbe huyo amewatolea mwito wananchi wa Somalia pamoja na makundi mengine yenye ushawishi kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha kwamba taifa hilo halirejei tena nyuma kwani kufanya hivyo ni kukaribisha janga lisilo na macho.