Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mbabe wa Kivita raia wa DRC Ahukumiwa Kifungo cha Miaka 14 Gerezani

Mbabe wa Kivita raia wa DRC Ahukumiwa Kifungo cha Miaka 14 Gerezani

 

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC imemhukumu mbabe wa kivita raia wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo Thomas Lubanga Miaka 14 gerezani baada ya kupatikana na makosa ya kuwaingiza watoto kwenye kundi lake la waasi kati ya mwaka 2002 na 2003.

Majaji kwenye kesi hiyo wanasema kuwa hata kama ni vigumu kubaini idadi ya watoto waliongizwa jeshini tabia hiyo ilikuwa imesambaa nchini DRC. Majaji hao waliongeza kuwa walitambua kipindi ambacho mshukiwa amekuwa kizuizi na tabia yake nzuri na kuafikia uamuzi huo ikimaaanisha kuwa Lubanga atatumikia kifungo cha miaka 8 gerezani. Adrian Fulford ni jaji kwenye kesi hiyo.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARDS)