Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban Asifu Uchaguzi uliofanyika katika Hali ya Amani Timor-Leste

Ban Asifu Uchaguzi uliofanyika katika Hali ya Amani Timor-Leste

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametuma salama zake za pongezi kwa wananchi wa Timor-Leste, serikali na makundi ya vyama vya kisiasa kwa kufanikisha uchaguzi wa bunge katika hali ya amani na utulivu mkubwa.

Ban katika salamu zake, amesema kuwa ametiwa moyo na kuhamasishwa namna wananchi wa taifa hilo walivyojitokeza na kufanikisha uchaguzi huo katika hali ya kuridhisha.

Taifa hilo liliendesha uchaguzi wa wabunge mwishoni mwa juma na kufungua ukurasa mpya wa kisiasa.

Ripoti za awali zinaonyesha kwamba chama cha Waziri Mkuu Xanana Gusmao kinaelekea kuibuka mshindi huku chama tawala, Fretilin kikisalia kwenye nafasi ya pili.