Sudan Kusini yaadhimisha Mwaka Mmoja tangu kupata Uhuru

9 Julai 2012

Kupitia usaidizi kutoka kwa shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP mengi kati ya majimbo kumi nchini Sudan Kusini yameboresha ukusanyaji wa ushuru kwa asilimia 100 baada ya kubuniwa idara za ukusanyaji wa ushuru.

Hii ni mojawapo ya hatua zilizizochukuliwa kuboresha ukusanyaji wa ushuru uamuzi uliotolewa baada ya kusitishwa shughuli za usafirishaji wa mafuta mwezi Januari mwaka huu shughuli iliyochangia karibu 98 ya pato la eneo hilo. Kwenye majimbo yote 10 UNDP imepeleka wataalamu ambao wamesaidia kutoa mafunzo kwa maafisa 490 wa kukusanya ushuru , wa masuala ya uhasibu na mipango ya maendeleo.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter