Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM kuchunguza Visa 200 dhidi ya Watu Kutoweka katika nchi 30

UM kuchunguza Visa 200 dhidi ya Watu Kutoweka katika nchi 30

Kundi la wataalam wa Umoja wa Mataifa kuhusu utowekaji wa kulazimu, limeanza kuchunguza tena zaidi ya visa 200 vya utowekaji kama huo. Visa hivyo vinahusisha baadhi ya visa chini ya mkakati wake wa visa vinavyohitaji hatua za dharura na habari kuhusu visa vipya na vya kale vinavyohusu nchi zaidi ya 30.

Wataalam hao huru watafanya mikutano na wawakilishi wa serikali na wawakilishi wa mashirika ya umma, pamoja na jamaa za watu ambao wametoweka, ili kubadilishana habari na mawazo kuhusu visa binafsi vinavyoshughulikiwa, na kuhusu suala zima la utowekaji wa watu wa lazima. George Njogopa anaripoti.

(RIOPOTI YA GEORGE NJOGOPA)