Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM Waitaka Ufilipino kuwalinda Wanaharakati wa Haki za Binadamu

UM Waitaka Ufilipino kuwalinda Wanaharakati wa Haki za Binadamu

Wataalam wawili wa Umoja wa Mataifa kuhusu wapiganaji wa haki za binadamu na mauaji kinyume sheria, wametoa wito kwa serikali ya Ufilipino kuweka mikakati ya dharura ili kulinda masilahi ya wanaharakati wa haki za binadamu na kuhakikisha kuwa wanaweza kutimiza majukumu yao.

Pia wameitaka serikali ya Ufilipino kufanya uchunguzi huru kwa haraka kuhusu idadi inayoongezeka ya matishio na mauaji ya wanaharakati wa haki za binadam, na kuwafikisha wahusika mbele ya sheria.

Habari za mauaji na vitisho kwa wanaharakati wa haki za binadam zimeongeseka maradufu katika miezi michache ilopita, hasa katika maeneo ya Mindanao na Mashariki mwa Visayas. Wamesema jamaa za wanaharakati hao pia zinakabiliwa na tishio la kuuawa. Wamesema visa vingi vya uhalifu dhidi ya wanaharakati wa haki za binadam vinawahusu wale wanaopigania haki ya watu kuwa na mazingira safi.

Wamesisitiza kuwa serikali ya Ufilipino ina wajibu wa kuwalinda watu wake, na inahitajika kuchukuwa hatua zifaazo kulinda haki na maisha ya watu.