Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la haki za binadamu la UM lamteua mjumbe maalum wa haki za binadamu na mazingira

Baraza la haki za binadamu la UM lamteua mjumbe maalum wa haki za binadamu na mazingira

Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limemteua John knox kama mjumbe maalum wa haki za binadamu na mazingira na pia kutangaza kundi la kushughulia ujenzi wa makao ya walowezi kiyahudi nchini Israel kabla ya kukamilika kwa kikao chake cha 20.

Uteuzi huo ulitangazwa na rais wa baraza la la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa Laura Dupuy Lasserre. Uteuzi wa knox unatokana na ujuzi wake katika masuala ya haki za binadamu , sheria ya mazingira ya kimataifa na masuala ya hali ya hewa. Bi Lasserre pia aliwateua Christine Chanet, Unity Dow na Asma Jahangir kuchunguza athari za ujenzi wa makao ya Israel kwa haki za kisiasa, kijamii na kiuchumi kwa watu wa Palestina.