Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lemke akarabisha uamuzi wa IFAB wa kuruhusu wanawakle kushiriki kwenye michezo

Lemke akarabisha uamuzi wa IFAB wa kuruhusu wanawakle kushiriki kwenye michezo

Mshauri maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu michezo kwa maendeleo na amani, Wilfried Lemke, amekaribisha uamuzi uliotolewa na bodi ya kandanda ya kimataifa IFAB kwa kuwaruhusu wanawake wanamichezo kuvaa hijabu iliyo salama kwenye michezo iliyo chini ya usimamizi wa shirika la kandanda duniani FIFA.

Amesema kuwa uamuzi huu ni hatua kubwa mbele ya kuhakikisha usawa kwenye michezo. Ameongeza kuwa uamuzi huu pia ni ishara kuwa kila mmoja duniani, awe wa kiwango cha aina gani, ana haki ya kushiriki michezo na kunufaika na yanayotokana na michezo