Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkurugenzi Mkuu wa IOM kutembelea Senegal

Mkurugenzi Mkuu wa IOM kutembelea Senegal

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM William Lacy Swing anatazamiwa kuwa na ziara ya kikazi Dakar Mji Mkuu wa Senegal ziara inayotazamiwa kuanza hapo jumatatu.

Akiwa nchini humo atahudhuria mkutano wa majadiliano ya wazi kwa nchi za afrika magharibi ulioandaliwa na jumuiya ya eneo hilo ECOWAS.

Mkutano huo unashabaha ya kuipa sura mpya taasisi ya kikanda ya eneo hilo MIDWA na kuboresha utendaji wake.

Akiwa nchini jijini humo balozi huyo anatazamiwa pia kukutana waziri mkuu AbdoulM'Baye na waziri wa mambo ya nje AlouineBadaraCissé.

Wote kwa pamoja wanatazamiwa kujadilia suala la kuboresha mahusiano mema baina ya IOM na Senegal