Pillay kuizuru Kyrgyzstan na Kazakhstan Julai 8-12

6 Julai 2012

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay anatarajiwa kufanya ziara yake ya kwanza eneo la Asia ya kati kuanzia tarehe 8- 12 mwezi huu.

Pillay ataanzia ziara yake nchini Kyrgyzstan ambapo shirika lake liliweka Ofisi mwaka 2008. Akiwa nchini humo Pillay anatarajiwa kukutana na rais Atambayev, mawaziri, mahakama, watetesi wa haki za binadamu na mashirika yasiyo ya kiserikali. Mnamo tarehe 10 mwezi huu Pillay atakuwa kwenye mji wa Osh ulio kusini – magharibi ambako alibuni ofisi kufuatia kuzuka ghasia za kikabilla za mwaka 2010 zilizosababisha vifo vya watu 400.

Kuanzia tarehe 11 mwezi huu Pillay ataanza ziara yake nchini Kazakhstan kwenye mji mkubwa zaidi nchini humo Almaty ambapo anatakutana na waziri wa mambo ya kigeni , mashirika ya umma na watetesi wa haki za binadamu kabla ya kusafiri kwenda mji mkuu.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter