UNHCR na washirika kuandaa mkutano wa kutafuta suluhu la makao kwa wakimbizi duniani.

6 Julai 2012

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR pamoja na washirika wengine wanakutana juma lijalo mjiji Geneva kutafuta njia za kuwasaidia wakimbzi 859,000 kote duniani ambapo makao yanatajwa kuwa suluhu pekee kwao.

Mkutano huo ambao utakuwa nchini ya uenyekiti wa Australia na kuleta pamoja waakilishi wa nchi zinazotoa makao, mashirika yasiyokuwa wa serikali na wafanyikazi wa UNHCR utajadili masuala kadha yakiwemo ushirikiano kwenye suala la kugawana mzigo wa kuwatafutia makao wakimbizi, kupunguza muda wa kuwatafutia makao wakimbizi hao na kuboresha njia za kuwapokea. Adrian Adward ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARD)

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter