Watoto waendelea kuingizwa jeshini kaskazini mwa Mali: UNICEF

6 Julai 2012

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF, linasema kuwa makundi yaliyojihami yanaendelea kuwaingiza kwenye jeshi watoto kwenye maeneo ya kaskazini mwa Mali.

UNICEF inaelezea hofu yake kuhusu hatma ya watoto kaskazini mwa Mali, kufuatia ripoti zinazosema kuwa kumeripotiwa visa ya ubakaji wa watoto wasichana.

Shirika hilo linasema kuwa ukosefu wa usalama umewalazimu karibu watoto 300,000 kuacha shule hali inayochangaia watoto hao kuingia jeshini. Marixie Mercado ni msemaji wa UNICEF mjini Geneva.

(SAUTI YA MARIXIE MERCADO)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud