Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO na washirika watoa ombi la msaada kusaidia mbuga ya wanyamapori iliyovamiwa na wawindaji nchini DRC

UNESCO na washirika watoa ombi la msaada kusaidia mbuga ya wanyamapori iliyovamiwa na wawindaji nchini DRC

Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO na shirika moja lisilokuwa la kiserikali wametoa wito wa msaada wa dharura utakaofadhili ujenzi wa mbuga moja ya wananyapori iliyovamiwa na wawindaji haramu nchini Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo.

Kulingana na UNESCO mbuga ya wanyamapori ya Okapi inayopatikana kwenye msitu wa Ituri ni makao kwa familia za wanyama zilizo kwenye hatari ya kuangamia zikiwemo ndege na twiga. Makao makuu ya mbuga hiyo yaliyo kwenye kijiji cha Epulu yalivamiwa mnamo tarehe 24 mwezi Juni na wawindaji haramu waliokuwa wamejihami vikali ambapo jumla ya watu saba waliuawa wakiwemo walinzi wawili wa mbuga waliuawa, nyumba kuteketezwa na jumla ya twiga 13 kuuawa