Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ahimiza ushirikiano na uiano kufikia Malengo ya Maendeleo

Ban ahimiza ushirikiano na uiano kufikia Malengo ya Maendeleo

Maendeleo yanaweza kupatikana tu kupitia ushirikiano na uiano, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, siku ya Alhamis kwenye ufunguzi wa kongamano la Baraza la masuala ya kiuchumi na ya kijamii ya Umoja wa Mataifa, ECOSOC kuhusu ushirikiano katika maendeleo.

Amesema mataifa yanayoendelea yanasaidiana kwa kutumia uzoefu yaliyonayo binafsi kuendeleza ushirikiano wa mataifa ya kusini mwa ulimwengu. Amesema mataifa hayo yanajenga mbinu za ushirikiano wa maendeleo, ambazo utekelezaji wake ni wa haraka na usiokuwa wa kupitia njia ndefu sana, na kwamba sekta ya kibinafsi imeonyesha kuwa mshirika muhimu, kama zilivyo hazina za maendeleo na sekta nyengine.

Ameongeza kuwa mashirika ya umma yanawasaidia walengwa kutumia vyema misaada ya maendeleo wanayopokea, na serikali za mitaa na mikoa zinasaidia kuwezesha utoaji wa huduma muhimu kama vile za afya na elimu. Amesema changamoto kubwa ni kuwa na uaino na utaratibu mwema miongoni mwa wahusika hawa wote.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)