Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwaka wa kwanza wa uhuru wa Sudan Kusini umekuwa wa changamoto kubwa:Johnson

Mwaka wa kwanza wa uhuru wa Sudan Kusini umekuwa wa changamoto kubwa:Johnson

Afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini amesema taifa hilo limepitia kipindi kigumu katika mwaka wake wa kwanza wa uhuru.

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini humo Hilda Johnson amewaambia waandishi wa habari mjini Nairobi Alhamisi kwamba Juba itaadhimisha mwaka wa kwanza wa uhuru kutoka Sudan Julai 9 huku ikiwa imeghubikwa na ghasia na mivutano na jirani zao wa Kaskazini.

Bi Johnson amesema mwaka huu unaomalizika umekuwa mgumu sana, wa machungu tele hasa kwa watu hao wa Sudan Kusini ambao walipaswa kujivunia na kusherehekea mafanikio ya kujitenga.

(SAUTI YA HILDA JOHNSON)