Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mood atoa hakikisho la kujitolea kwa UM nchini Syria

Mood atoa hakikisho la kujitolea kwa UM nchini Syria

Mkuu wa kundi la Umoja wa Mataifa nchini Syria Meja jenerali Robert Mood hii leo amekutana na naibu Waziri wa mambo ya kigeni nchini Syria.

Akihutubia waandishi wa habari baada ya mkutano huo Mood aliwakumbusha waandishi hao kuwa oparesheni ya Umoja wa Mataifa nchini Syria ilisitishwa tarehe 15 mwezi Juni.

Amesema kuwa viwango vya juu vya machafuko nchini Syria vimetatiza juhudi za Umoja wa Mataifa kutekeleza wajibu wake nchini humo. Aliwakikishia watu wa Syria kuwa UM wa Mataifa utaendelea na juhudi zake za kuwasaidia.

(SAUTI YA MEJA JENERALI MOOD)