Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO na FAO waweka viwango vipya vya ubora wa bidhaa

WHO na FAO waweka viwango vipya vya ubora wa bidhaa

Shirika la Umoja wa Mataifa la kukadiria ubora wa bidhaa limekubali kuweka viwango vipya vyenye lengo la kulinda afya za wanaotumia bidhaa hizo kote duniani. Kati ya viwango vilivyoweka ni pamoja na kiwango cha kemikali ya melamine kinachowekwa kwenye maziwa ya watoto.

Viwango hivo vipya vilikubaliwa wakati wa mkutano wa tume ijulikanayo kama Codex Alimentarius iliyo na jukumu la kukadiria ubora wa vyakula duniani. Kemikali ya melamine imekuwa ikiongezwa kwenye maziwa kwa minajili ya kuongeza madini ya protini kwenye maziwa ya watoto.

Mwaka 2008 watoto kadhaa walikufa nchini China baada ya kunywa maziwa yaliyokuwa yameongezwa melamine na sasa tume hiyo imepunguza kiwango chake kwenye maziwa toka miligramu moja kwa kila kilo moja ya maziwa hadi miligramu 0.15 kwa kila kilo ya mziwa.