Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais wa Baraza Kuu alaani Mashambulizi ya Makanisa nchini Kenya

Rais wa Baraza Kuu alaani Mashambulizi ya Makanisa nchini Kenya

Rais wa Baraza Kuu,  Nassir Abdulaziz Al-Nasser amelaani mashambulizi ya mwishoni mwa wiliki iliopita katika makanisa mawili mjini Garissa, Kenya. Mashambulizi haya ambayo yalilenga maeneo ya kuabudu, yalisababisha vifo vya watu 17 na kujeruhi watu wengine kadhaa.

Rais Al-Nasser amesisitiza umuhimu wa kuwepo kwa usalama katika maeneo yote ya kuabudu na usalama wa wote wanaoabudu bila kujali dini yao.

Rais huyo wa Baraza Kuu ametoa rambi rambi zake kwa familia ya waathirika, serikali na watu wa Kenya.