Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Navi Pillay alitaka Baraza la Usalama Kuwasilisha Mzozo wa Syria kwenye Mahakama ya Kimataifa ICC

Navi Pillay alitaka Baraza la Usalama Kuwasilisha Mzozo wa Syria kwenye Mahakama ya Kimataifa ICC

Mkuu wa kamishna ya Umoja wa Mataifa juu ya masuala ya haki za binadamu amerejelea wito akilitaka baraza la usalama kuwasilisha mzozo wa Syria katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC akisisitza kuwa ni lazima wahusika wa machafuko hayo wanawajibishwa.

Navi Pillay amewaambia waandishi wa habari baada ya kuwa na kikao cha ndani na baraza hilo la usalama kuwa pande zote kwenye mzozo huo zinapaswa kuwajibika. Amesema vikosi vya serikali pamoja na vile vya waasi haviwezi kujiweka kando na madhira ya mzozo huo kwani kila upande umeshiriki kwenye matukio ya kuwashambulia raia.

Ametaka wale wote waliohusika na mashambulizi dhidi ya raia lazima wawajibishwe kwenye mkono wa sheria na amelitolea mwito baraza la usalama kuwasilisha mzozo huo kwenye mahakama ya kimataifa ICC.