Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM na UNHCR waanzisha Mradi Kuwakwamua raia wa Iraq Waliokosa Makazi

IOM na UNHCR waanzisha Mradi Kuwakwamua raia wa Iraq Waliokosa Makazi

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yamezindua mpango wenye shabaha ya kuzisaidia zaidi ya familia 900 nchini Iraq ambazo zilikwenda mtawanyikoni.

Mashirika hayo lile la kushughulikia wakimbizi UNHCR pamoja na lile la uhamiaji IOM yameanzisha mpango huo wa miezi sita ambao utatoa fursa kwa familia hizo kufungamanishwa katika maeneo ya uchumi jamii.

Ndani ya mpango huo kiasi cha dola za kimarekani 650,000 kimetengwa ambacho kitatumika kufadhilia ujenzi wa nyumba rafiki kwa mazingira.

Mashirika hayo tayari yamefanya utambuzi kwa familia zinazoandamwa na hali ngumu zaidi ambazo ndizo zitazopewa kipaumbele wakati wa utekelezwaji wa mradi huo utakaofikia ukomo wake mwezi disemba.