Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM Yajenga Kambi kwa Wanajeshi na Familia zao nchini DRC

IOM Yajenga Kambi kwa Wanajeshi na Familia zao nchini DRC

Kambi mbili zilizojengwa na shirika la kimataifa la uhamiaji IOM kuwapa makao wanajeshi 1,038 na familia zao zimefunguliwa rasmi eneo la Kivu Kusini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Uzinduzi wa mradi huo uliofadhiliwa na serikali ya uholanzi kwa gharama ya dola milioni 11 ulihudhuriwa mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Roger Meece na mabalozi wa uholanzi na muungano wa Ulaya.

IOM ilianzisha ujenzi wa makambi hayo mwaka 2009 kwa lengo la kuzisaidia familia za wanajeshi ambazo zimekuwa zikiishi kwenye mahema kwa miaka mingi na kudumisha nidhamu jeshini. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMAR JUMBE)