Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mgogoro wa Syria Unazidi kuwa wa Kidini:Pillay

Mgogoro wa Syria Unazidi kuwa wa Kidini:Pillay

Kamishina Mkuu wa haki za binadamu Navi Pillay akihudumia baraza la haki za binadamu Jumatatu amesema mgogoro wa Syria unazidi kuwa wa kidini na taratibu kuigawanya jamii.

Pia amesema ukosefu wa ulinzi kwa raia nchini humo unaongezeka huku idadi ya vifo ikipanda na fursa ya kufikisha misaada ya kibinadamu na huduma zingine muhimu kwa waathirika wa vita ikipungua.Kuhusu suala la endapo ni vita au la amesema katika baadhi ya maeneo kuna ishara kwamba hali ya Syria sio vita vya kimataifa au vita vya ndani. Msemaji wake Rupert Colville amewaelezea waandishi wa habari kuhusu hofu ya Pillay.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)