Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushirikiano wa Kimatifa kwa Ajili ya Maendeleo ni Muhimu Kufikia Malengo ya Milenia

Ushirikiano wa Kimatifa kwa Ajili ya Maendeleo ni Muhimu Kufikia Malengo ya Milenia

Malengo muhimu matatu ya milenia yamefikiwa miaka mitatu kabla ya wakati ambayo ni umasikini, mitaa ya mabanda na maji, imesema ripoti ya ya malengo ya maendeleo ya milenia iliyozinduliwa leo na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon.

Ban amesema ingawa kufikia malengo mengine yaliyosalia ni changamoto, itawezekana tuu kuyafikia ikiwa serikali zitatimiza majukumu yake zilizojiwekea muongo mmoja uliopita. Ameongeza kuwa mafanikio zaidi yatapatikana kwa kuzingatia utumizaji wa lengo namba 8 ambalo ni ushirikiano wa kimataifa wa maendeleo.

Ripoti hiyo imesema kwa mara ya kwanza tangu mwenendo wa umasikini umekuwa ukifuatiliwa idadi ya watu wanaoishi katika umasikini uliokithiri na kiwango cha umasikini vimepungua ikiwemo katika nchi za Afrika zilizoko kusini mwa jangwa la Sahara ambako kiwango cha umasikini kilikuwa cha juu sana.