Wengi Wameathiriwa Machafuko ya Rakhine, Myamar:OCHA

29 Juni 2012

Kiasi cha watu 78 wamepoteza maisha na wengine 87 wamejeruhiwa wakati kulipozuka machafuko katika jimbo la Rakhine liliko nchini Myanmar.

Takwimu hizo ni kwa mujibu wa ofisi za Umoja wa Mataifa zinazoshughulikia na masuala ya usamaria mwema OCHA kama ilivyozinukuu toka wizara ya habari ya nchini humo.

Kiasi cha nyumba 3000 ziliharibiwa na kubomolewa wakati wa machafuko hayo yaliyozuka mwezi June mwaka huu ambayo pia yamesababisha zaidi ya watu 52,000 kukosa makazi.

Serikali imeanzisha mpango wa kutoa misaada ya dharura kwa waathirika wa matukio hayo ikiwemo pia kutoa makazi ya muda kwa wale waliyovunjiwa nyumba zao

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter