Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Amos aelezea Wasi Wasi Wake Kutokana na Hali ya Wakimbizi nchini Sudan Kusini

Amos aelezea Wasi Wasi Wake Kutokana na Hali ya Wakimbizi nchini Sudan Kusini

Mratibu wa huduma za dharura kwenye Umoja wa Mataifa Valerie Amos ameelezea wasi wasi uliopo kutokana na kuendelea kuzorota kwa hali ya kibinadamu kwenye majimbo ya Kordofan Kusini na Blue Nile nchini Sudan.

Taarifa kutoka kwa Ofisi ya Amos inasema kuwa maelfu ya watu wamekwama kwenye eneo la mzozo wakiwa hawana chakula, maji , makao na huduma za afya. Inaendelea kusema kuwa Maelfu ya wengine wanaendelea kuvuka mipaka na kuingia mataifa jirani kila siku wakikimbia mapigano na kutafuta chakula. Tangu mwezi Aprili idadi ya wakimbizi kutoka Sudan wanaowasili nchini Sudan kusini na Ethiopia imeongezeka maradufu hadi wakimbizi 200,000.