IOM yachimba Visima na Kujenga Matenki ya Maji kwenye Kambi ya Wakimbizi ya Doro Sudan Kusini

29 Juni 2012

Shirika la la kimataifa la uhamiaji IOM limeanzisha zoezi la uchimbaji visima na kujenga jumla ya matenki mawili kwa minajili ya kuwahakikishia maji takriban wakimbizi 42,000 kwenye kambi ya Doro kwenye jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini. Inakadiriwa kuwa watu 107,000 wamevuka mpaka na kuingia jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini na sasa wanaishi kwenye kambi zikiwemo kambi ya Doro, Jamam na Yusif Batil.

Doro ambayo ndiyo kambi kubwa zaidi kati ya kambi zote tatu iko umbali wa kilomita 20 kusini mashariki mwa kambi ya Yusif Batil iliyobuniwa kuwapokea wakimbzi 23,000 kutoka kituo cha Kilo 18. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMAR JUMBE)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter